Post by Yona Maro on Oct 11, 2005 6:33:36 GMT -5
ELIMU-BURKINA FASO:
Ukitaka Kupanua Elimu, Tumia Lugha Ya Kizalendo
Tiego Tiemtore
OUAGADOUGOU, Sep 19 (IPS) - Mwaka 1990, mtaalamu wa lugha nchini Burkina Faso, Benoit Ouoba alitumia fedha zake kuanzisha mpango wa pekee: wenye lengo la kutumia lugha ya kizalendo kuendeleza elimu, badala ya lugha iliyozoeleka ya Kifaransa.
Miaka kumi na tano baadae, mbinu ya ‘Tin Tua’ ilitumika kufundishia sehemu ya mashariki ya jimbo la Gulmu mahali ulipoanza kutumika, na kuvutia wafadhili wengi wakati huo.
Tin Tua, ikiwa na maana ya ‘Twende Tukajiendeleze Wenyewe’, umechukuliwa kutoka kabila la Gulmancema – miongoni mwa makabila ya kizalendo yanayotumika nchini Burkina Faso.
Mfumo huo wa ufundishaji unamtaka mwanafunzi apate elimu kwa lugha ya Gulmancema – au lugha nyingine ya kizalendo kama ya Fulfulde, Moore au Haussa – kabla ya kuendelea na masomo mengine kwa Kifaransa. Mfumo huo unaenda kwa pamoja na jitihada za kuhifadhi ufahamu wa mwanafunzi katika mila kwa kuwapatia hadithi nyingi za kitamaduni na kizalendo.
Mpango huo unaendeshwa katika rika zote. Kwa mujibu wa Ouoba, karibu kila theluthi moja ya idadi ya watu wazima wa Gulmu imepitia katika vituo vya elimu vya Tin Tua, kwa uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume. Vituo hivyo vinaitwa "Banma Nuara" – kwa maana nyingine ya Gulmancema ikimaanisha "Amka".
"Watu wazima ambao hawawezi kuendelea na elimu ya juu ya sekondari basi hujua kusoma na kuandika kwa lugha yao. Ni maendeleo makubwa," Moussa Sanou, mtaalamu wa lugha kutoka Chuo Kikuu cha Montreal nchini Canada, ameliambia shirika la habari la IPS.
Sanou anafanya utafiti nchini Burkina Faso kuhusu mahusiano kati ya lugha ya Kifaransa na lugha za kienyeji za Burkinabe.
Mwaka 1992, mradi wa Tin Tua ulianzisha gazeti liitwalo ‘Laabaali’, maana yake "Habari" katika lugha kadha za kizalendo Magharibi mwa Afrika. Gazeti hilo huchapisha makala katika lugha za kienyeji ili kutoa fursa kwa wale waliojifunza kusoma katika lugha hizo waweze kudumisha ujuzi wao.
Mafanikio ya Tin Tua yanajidhihirisha kutokana na kufaulu kwa kiwango cha juu kwa wanafunzi wanaofanya mitihani ya kitaifa ya elimu ya msingi. Watu wengi pia wameweza kupata sifa za shule ya sekondari.
Wale ambao umri wao ni wa utu uzima wanaweza kupata fursa katika chuo kilichofunguliwa na Tin Tua mwaka 2004 kwa kutoa masomo ya kilimo, ufugaji na upandikizaji. Wanafunzi pia hufundishwa hesabu na misingi ya uchumi, na wanajifunza pia usafi na mazingira.
Wakati huo huo, ratiba ya kozi hutoa nafasi ya ziada kwa wanafunzi kushiriki katika shughuli za kutafuta kipato, kama kutengeneza sabuni.
"Nafikiri mfano wa Tin Tua ni wa kuigwa. Serikali itajiunga na washirika wote kutoka sekta za ufundi na uhasibu kueneza mpango huo katika kila jimbo," Waziri Mkuu Ernest Paramanga Yonli amesema mapema mwaka huu wakati wa sherehe za kutimiza miaka kumi na tano ya Tin Tua.
Kusema kweli, Tin Tua imeanza kuzaa matunda yake katika mfumo wa elimu ya kitaifa. Zaidi ya miaka kumi iliyopita, ni madarasa mawili tu katika nchi nzima yalikuwa yakifundishwa kwa lugha zote mbili, kizalendo na kifaransa. Leo, shule nyingi za msingi zinafundisha kwa kutumia lugha zote mbili – ingawaje mfumo huo bado haujafika katika shule za sekondari.
Asilimia tisini ya mafunzo hayo katika shule hizo za msingi huendesha kwa lugha ya kienyeji kwa kuanzia – na asilimia 10 iliyobaki kwa Kifaransa. Kifaransa hutumika zaidi katika miaka mitano inayofuatia, hadi pale mafunzo yanapoendeshwa kwa Kifaransa kwa asilimia 90 – na asilimia 10 kwa lugha za kizalendo.
Walimu hupata mfunzo ya mara kwa mara ya kufundisha kwa kutumia lugha hizo.
Vile vile, kiwango cha mafanikio cha wanafunzi wanaofanya mitihani ya kitaifa kutoka shule hizi ni ushahidi wa kutosha wa matunda ya kufundishia lugha mbili. Zaidi ya asilimia 94 ya wanafunzi wamefaulu majaribio mwaka 2004, wakati karibu asilimia 74 wamefaulu mitihani ya kitaifa.
"Faida ya kutumia lugha za kizalendo katika kufundisha ni kwamba inatoa nafasi ya kujifunza," anasema Sanou. "Kwa kutumia lugha za kizalendo, watoto wanajifunza haraka sana. Unaweza kufundisha masomo ya shule ya msingi kwa miaka mitano badala ya sita."
Hata hivyo, kiwango cha juu cha kufaulu katika shule zinazotumia lugha mbili bado hazijashawishi watu wote.
"Nafikiri faida yake ni ya kizalendo…Nje ya Burkina, utaitumiaje lugha ya kienyeji? Unaweza kumpelekea mtu barua pepe katika lugha ya Moore au Gulmancema?" anauliza Nestor Coulibaly, mwalimu katika shule inayofundisha kwa lugha mbili kaskazini mwa nchi hiyo.
Hata hivyo, Sanou analinda mfumo huo wa matumizi ya lugha mbili: "Ili klleta demokrasia katika elimu barani Afrika, tunahitaji kutafuta mkakati wa kutumia lugha za kizalendo kufundishia."
Njia ya kufundishia ya The Tin Tua inaweza kuenea zaidi ya mipaka ya Gulmu, hasa kwa serikali ambazo zinapata changamoto za kutoa elimu ya msingi kwa wote ifikapo 2015.
Hili ni moja kati ya malengo nane ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), yaliyokubaliwa na viongozi wa mataifa katika Mkutano wa Milenia mwaka 2000. Malengo ya Maendeleo ya Milenia pia yanaangalia – kwa sehemu – kupunguza umaskini uliokithiri kwa nusu na kupunguza vifo vya watoto na uzazi. (END/2005)
www.ipsnews.net/africa/sw/interna.asp?idnews=1075