|
Lugha
Oct 11, 2005 6:28:00 GMT -5
Post by Yona Maro on Oct 11, 2005 6:28:00 GMT -5
Lugha ni utaratibu kwa ajili ya kuwasiliana kati ya binadamu au kati ya viumbe wo wote wenye akili. Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu. Maana ya neno "lugha" Mara chache neno lugha linatumika kwa taratibu za kuwasiliana za wanyama. Lakini taratibu hizo ni tofauti sana: Katika lugha za wanyama, sauti moja ina maana moja tu. Lakini katika lugha za binadamu, sauti nyingi zinaunganishwa kutengeneza maneno, na maneno mengi yanaunganishwa kutengeneza sentensi. Hivyo mnyama ambaye anaweza kutengeneza sauti ishirini tofauti anaweza "kusema" mambo ishirini tu. Kwa upande mwingine mtu ambaye anaweza kutengeneza sauti ishirini, anaweza kusema mambo zaidi ya bilioni. sw.wikipedia.org/wiki/Lugha
|
|