|
Post by Yona Maro on Oct 5, 2005 0:10:34 GMT -5
Ngoja nikupe hadithi moja hivi, Kuna dada mmoja, alikua njiani wakati wa kwenda kazini, wakati akiwa kwenye kituo cha basi mara akatokea kaka mmoja akamwambi yule dada kua apande kwenye gari kwani na yeye anaelekea hukohuko anakoenda huyo dada. Yule dada akapanda lakini cha kushangaza ni kua yule kaka alianza kuendesha gari kwa kasi kuliko ilivyokua mwanzo. Sasa walipofika eneo lile yule dada anaposhukia akamwambia samahani kaka nimeshafika naomba unishushe. yule kaka hakumjibu bali alizidi kuendesha gari kwa kasi Mara wakaingia kwenye nyumba moja kubwa akamshusha yule dada na kumkaribisha sebuleni, yule kaka akaenda ndani akarudi na kobe na kumwambia kua amnyonyeshe mapaka ashibe huku akiwa ameshikiwa bastola. Baada ya yule kobe kushiba aliacha mwenyewe kunyonya na ndipo yule kaka alimruhusu yule dada kuondoka Alienda nyumbani kwao kwa kusaidiwa na watu kwani alikua anasikia kizunguzungu, alipofika alimhadithia mama yake mkasa wote ulio mpata, na baada yahapo alidondoka chini, alipelekwa hospitali na alipopimwa alionekana hana damu hata kidogo na akafariki dunia . Kwahiyo ndio maana ninakuambia kuamakini sana na unachokifanya yasije yakakutokea yaliomtoke huyu dada
|
|
|
Post by malisak on Oct 10, 2005 5:07:09 GMT -5
yona maro hiyo story ni kweli kabisa tena ilitokea mkoani arusha ila huyo dada hakua akienda job alikua akienda uwanja wa sabasaba kwenye maonesho ya nane nane ni kweli tupu tena hiyo story imevuma sana Arusha.
|
|
|
Post by Yona Maro on Oct 10, 2005 9:07:38 GMT -5
WOW AHSANTE KWA KUTOWA TAARIFA ZAIDI HIYO HADITHI MIMI PIA NILIAMBIWA NA RAFIK YANGU MKAZI WA HUKO HUKO ARUSHA KWAHIYO SIKUWA NA UHAKIKA SANA HADITHI YENYEWE KUMBE NI KWELI .
POLE KWA KINA DADA ILA HIYO NI FUNDISHO
|
|