Post by Yona Maro on Oct 3, 2005 8:02:29 GMT -5
Habari
Hadithi hii ilininutsuwa na kunisikitisha , hadithi hii ni ya kweli kabisa lakini kwa sababu za binafsi majina ya wahusika nitaficha na kutumia majina tofauti , ninachotaka ni ujumbe ufike kwa jamii husika tu , basin a hiyo jamii husika ijifunze kitu Fulani katika maisha yao ya kila siku , wakati wewe unahangaika kutengeneza maisha yako na jamii yako , kuna wengine wanahangaika kuja kukuharibia maisha yako tena kwa makusudi ndio mkasa huu hapa chini .
Bwana joni aliowa zaidi ya mara 2 na hapo wake zake wote hao 2 walifariki dunia akampata mke wa tatu , huyu mke wa 3 ndio ndugu yake na huyu dada aliyenipa mkasa huu , dada huyu anaitwa grace , grace anamiaka 39 sasa hataki kusikia cha uchumba wala unyumba yeye anajifunza kutokana na dada yake alivyofanyiwa , anapenda maisha salama nay a haki mbele ya kila mtu .
Kwahiyo dada yake grace kwa jina la LEA aliolewa na Joni , leo hakujua chochote kuhusu lea , hakujua maisha yake yalikuwaje , wakati huo joni alikuwa amepanga , basi bwana joni sijui hela alizifuma wapi , akajenga nyumba chap chap huko mbezi kimara , lea hajui chochote kuhusu joni yeye anajua joni anafanya kazi tu , lakini hajui kazi gani na wapi , alimwona joni na magari ya kifahari .
Joni na Lea wakapata watoto 2 mmoja alikuwa vizuri sasa huyu mtoto wa 2 alipofikisha miaka 5 akaanza kuumwa magonjwa ya ajabu ajabu , mara kifua mara malaria mara sijui nini , alifika siku zake , mtoto wa wa miaka 5 alifariki dunia akazikwa , hapo siri hazijulikani alikufa kwa nini hasa , mwenye siri hii ni joni baba mzazi wa mwana .
Baadaye lea naye akaanza kuumwa , aliumwa mpaka akawa anazimia , kazini na kupelekwa hospitali , alipimwa magonjwa mengi sana tena yote , kumbe akienda kupimwa , kijana joni anawaambia madaktari wasiseme kama leo anaukimwi wala yeye , waseme vitu vingine tu , bado joni anaweza siri zake mwenyewe , lea aliptwa na majipu na vidonda mwilini , ndugu zake wakimtembelea wanalia sana ndugu yao waliyempenda sana ndio anaenda hivyo .
Lea aliaga dunia , joni akajioni mpweke , hakuvumilia akaenda kutafuta msichana mwingine anayeishi mbezi beach , huku alimpata mwingine anaitwa lulu , joni akatangaza anaowa mke mwingine , ndugu na jamaa walifanya maandalizi ya harusi na kadhalika , grace alishajua kwamba joni anangoma , alienda nyumbani kwa akini lulu na kutowa taarifa hizo , wakina lulu na wazazi wake hawakuelewa .
Wakapanga ndowa wakafunga hiyo ndoa kwa pombe na majigambo kibao , sasa hivi naye lulu ameanza kuumwa , mwaka mmoja tu tangia wafunge ndoa na hali yake ni mbaya sasa yuko kitandani hajiwezi , kijana joni bado anatesa , yeye hutumia vidonge maalumu kwa ajili ya afya yake , vidonge hivi ni bei ghali hawezi kununua vingi kwahiyo ni yeye mwenyewe .
Lea hakutaka kumjua joni vizuri kabla ya kuolewa , akaona ,madhara yake , lulu naye hakutaka kusikia wala kuambiwa sasa hivi nay eye anaumwa sana , hajitambui , dalili za ukimwi anazo hakuna ubishi , na wazazi wa lulu wana wasisi na mwanao .
Wazazi wa lulu wakaamua kumwambia joni akapime ukimwi yeye na lulu wake , lakini wameshachelewa sana , yaani lulu anaumwa ndio munanutsuka mambo ya kupima ukimwi kama sio ukichaa ni nini ?
Joni akiambiwa akapime ukimwi huwa anamwita baba yake anayeishi bukoba , huyu baba ni daktari maarufu pale muhimbili , kwahiyo baba yake huja huku na kuwahonga wale wapimaji , ndio walivyofanya kwa lea na hata kwa lulu , wakaonekana hawana ukimwi .
Watu kama hawa wakina joni , na kina lulu na lea wako wengi sana , wakina lulu , lea hawaamini kama wakina joni wanaumwa , kwa sababu wanaona pajero yake , mali zake na kadhalika , lakini wakina joni wanajijuwa wanaumwa lakini anataka kukomesha tu .
Haya ndio maisha , nap engine mimi na wewe tuko katika mtego huo huo , ni vuzuri tujiangalie na tujikinge kama grace alivyofanya au pengine kuliko grace , grace alifanya vizuri lakini alipuuzwa wakina grace wako wengi sana , ukiwa kama grace unaonekana wewe unawivu wanaweza kukuambiya unataka kuvunja ndoa za watu ila huo ndio ukweli .
Nakutakia maisha mema , ila jitunze utunzike , kama huwezi karibu kidogo kidogo mpaka ufanikiwe , hakuna asiyependa kuishi maisha mazuri , bila magonjwa , bila hofu bila matatizo na watu , kila mtu anapenda amani , utulivu na uhuru wa kweli .
Maisha haya mhh sijui tutafika wapi .