|
Post by Yona Maro on Oct 1, 2005 1:01:46 GMT -5
Leo nimeruka tena siko upande wa siasa wala IT kwa mara nyingine , niko upande wa wazazi na malezi yao kwa watoto wao hasa watoto wa kike , watoto wa kike ndio wanatakiwa kutunzwa zaidi na kuwa karibu zaidi kwa sababu watu wengi huwazonga wao zaidi katika kufanikisha tama zao hasa za kimwili . Nimeona kuongelea suala hili tete kutokana na kusoma magazeti kadhaa leo asubuhi , wahariri wengi wanalala mika kuhusu wanafunzi wa chuo hasa wa mwaka wa kwanza kutokuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya matumizi yao wakiwa chuoni , yaani kula kwa siku mara 3 , malazi na kadhalika , wengi wanaitupia serikali ya jamhuri wa muungano wa Tanzania dhambi hizo , yaani wanailaumu serikali . Basi nikaanza kuwauliza marafiki zangu wanaosoma kule kwa njia ya SMS kujua kinachoendelea nao wakaniambia hivyo hivyo kwamba fedha hawajapewa bado na masomo yameshaanza , kuna wanafunzi wanadiriki kujiuza ili kupata fedha kwa matumizi ya kila siku , wengine wanasaidiwa na wahadhiri wa chuo kikuu , wengine wanasaidiwa na rafiki zao na kadhalika . Hii ni aibu kubwa tena kwa chuo kikubwa kwa Tanzania kama UDSM sasa huko Iringa napo pakoje kama hapa ni hivi au huko mwanza nako pamoje au serikali inajali kule zaidi ya hapa UDSM ? na lingine kujiuliza hivi wazazi wanavyoamua kuzaa watoto na kuwalea mpaka hapo walipo kama miaka 18 na kuendelea wanafikiria nini yaani wanashindwa hata kumuandalia mtoto wake fungu la fedha kidogo la kuanzia maisha ya chuo ?
|
|
|
Post by mwendapole on Oct 3, 2005 6:56:28 GMT -5
Mara nyingi hakuna mzazi anayetaka kumuona mtoto wake akiwa na tabia mbaya au ameharibikiwa kimaisha, kila mzazi anategea kua leo na kesho mtoto wake awe daktari, mhasibu, mwalimu na kadhalika
Tatizo linakuja kwa watoto wenyewe wanapofika huko vyuoni na kuwaona wenzao kila siku wanakula chips kuku, wanavaa nguo za kileo, anapojlinganisha na wenzake na kuona tofauti ndipo anajisahau kua amekuja tu kusoma na sio kwa ajili ya mashindano ya nguo na urembo.
Wazazi wananyima sana ili angalau watoto wao wapate elimu bora na wafanikiwe baadae shida ipo kwa watoto wenyewe.
|
|