Post by Yona Maro on Oct 20, 2005 6:56:17 GMT -5
Hadithi hadithi
Hapo zamani kulitokea jamaa mmoja na familia yake , maeneo ya kimara stop over , wazee hawa wakichaga walipenda kufuga mifugo kwao , moja ya mifugo hiyo ni nguruwe , walifanikiwa kutunza sana nguruwe wao mpaka wakazaliana , waliwauza kwa watu na wakapata faida kubwa sana , Maishani mwao na katika familia yao .
Siku zote , palipo na fedha au rasilimali wezi hawakosekani , basi bwana kipindi kikafika mzee ringo akiamka asubuhi anakuta nguruwe 2 hawapo , akitembea kidogo anakuta manyoya ya nguruwe kana kwamba wamechinjwa usiku ule , alianza kufukuza wafanyakazi wake , akifikiri kwamba wale ndio wezi wa nguruwe wake .
Kwa muda wa wiki 3 hivi kila siku ni nguruwe 2 alikuwa wakiibiwa usiku na kuchinjwa hapo hapo nyumbani kwake , bila yeye kujuwa wala walinzi wake , mzee ringo haamini kinachotokea , lakini alikuwa na pupa sana mara afukuze wafanya kazi na kadhalika , hayo ndio maisha .
Basi siku moja akatoka nje kwa majirani zake kuwauliza kuhusu nuguruwe wake wanaoibiwa kila kukicha , je kama watu wanamwonage mtu yoyote akitoka nyumbani kwake asubuhi sana ? Jirani wakamwambia kwamba , kuna kujana huwa anatoka humu kwako mida ya saa 11 asubuhi amevaa kanzu kama anakwenda msikitini , lakini huwa ana kiroba amebeba .
Mzee ringo akasikia hiyo lakini bado haamini , yaani nguruwe walivyokuwa wakorofi vile wanabebwa na kuchinjwa nyumbani kwake bila kupiga kelele na bila mtu yoyote kujua ? Lazima kuna mkono wa mtu hapa , au wanakimzizi nini hawa jamaa wanaoiba nduruwe zetu , aseee MANGI , RUA MUNGU .
Siku hiyo mzee ringo na vijana wake na hasira zao wakaamka asubuhi asubuhi , kwenda pale pale kwenye kona ambayo kijana muiba nguruwe hupitaga ,
Ghafla wakamwona kijana mmoja mtanashati , amevaa kanzu lake , kibagarashia , mustachi wa nguvu , bila kusahau kiroba nyuma yake amebeba , mambo yalikuwa matamu .
Ringo : Samahani kijana Umebeba nini , tunaweza kuona ?
Mwizi : Mzee nimefunga swaumu usinisumbuwe naenda msikitini kumwomba mola
Ringo : Mimi nauliza huko nyuma una nini ?
Mwizi : Nyuma wapi ? Nyuma nini makalio wewe umeona nini zaidi ? Mbona unanipa stimu ?
Ringo :Eeeh kwahiyo hicho ulicho beba bi makalio sio ?
Mwizi : Sijababe makalio nimebeba mkeka wa kwenda msikitini kama umeona nimebeba makalio basi njoo uyachukuwe ! Sura kama Birika
Ringo ; Yaani kijana umeanza kunitukana hivi hivi mi nakuuliza maswali unanitukana hivi hivi ?
Mwizi : Sijakutukana mie nakupa live , wewe ulifikiri nimebeba nini ? Hebu niache niishie zangu masjid .
Mzee ringo uzalendo ulimshinda akamkimbiza na kuchukuwa lile fuko , jamaa wengine walimkamata yule kijana , basi walipoangalia ni kweli walikuta nyama za nguruwe kule ndani ya fuko .
Watu wakaanza kumpiga yule kijana , asubuhi ile mpaka mwisho wa maisha yake .
Na huo ndio ulikuwa mwisho wa kijana Mwizi
Na mwisho wa hadithi yaa ya mwizi