|
Post by Yona Maro on Oct 17, 2005 8:28:19 GMT -5
Unajisikiaje ukiona Baba yake unayemtegemea kwa vitu vingine au pengine aliyekulea na kukutunza wakati wote wa utoto mpaka ujana akafariki ?
Unajisikiaje , mama yako aliyekutunza kwa miezi 9 tumboni mwake kisha akakuzaa , akakunyonyesha na kukulisha , akakutunza kujuwa mabaya na mazuri , na kukusaidia katika masomo naye amefariki ?
Utajisikiaje , kama mtu unayempenda kuliko wote , mchumba wako au rafiki yako naye akafariki dunia ?
Pia utajisikiaje , ndugu zako wote wakafariki dunia ? kwa kufuatana leo yule kesho yule ?
Halafu hawa wote , ndugu zako na mama yako na baba yako na mchumba wako wamefariki kwa ugonjwa wa UKIMWI ?
Ndio inawezekana utajisikia vibaya baadaye machungu yakaisha lakini kidonda kiko pale pale , kitaendelea kuambukiza watu wengine na wewe mwenyewe binafsi utafariki kwa ugonjwa huo huo .
Kwahiyo kijana mwenzangu , Mwanadamu mwenzangu , Tuwe makini na maisha yetu na maisha yaw engine tunaowajali na hata tusio wajali , katika amani , upendo na uhuru sisi wote ni sawa .
UKIMWI UPO , NA UTAENDELEA KUWEPO NA KUUWA VIZAZI , WEWE PIA UNAWEZA KUJIZUIA NA KUZUIA WENGINE WASIAMBUKIZWE .
MI NIMEPOTEZA MAMA YANGU MDOGO KWA UGONJWA HUU , HADITHI YAKE NDEFU , NILIOGOPA KUMSOGELEA .
NINAYAPENDA MAISHA YAKO , NAPENDA UISHI SALAMA NA UWE NA TUMAINI JEMA KWAKO .
|
|