|
Post by Yona Maro on Aug 30, 2005 7:55:18 GMT -5
Kuna jamaa mmoja alikuwa anampa ombaomba pesa kila siku, ila idadi anayompa ikawa inapungua mwaka hadi mwaka, yule ombaomba siku moja akasema lazima nimtolee uvivu huyu mtu, kila baada ya mwaka anapunguza kiasi, siku moja ikawa hivi: Ombaomba: Nashukuru unanisaidia kila siku ila nataka nijue kwa nini hela inapungua taratibu? Msamaria:Unajua wakati nakupa hela nyingi nilikuwa sina mke wala mtoto, baada ya hapo nikaoa, na baadaye nikapata mtoto wa kwanza na baadaye wa pili, ndio maana hela inapungua, Ombaomba: Pambafu! yaani unatumia hela yangu kulelea familia yako!
|
|