Post by Yona Maro on Dec 11, 2005 6:17:36 GMT -5
MEI 31 ni Siku ya Kutovuta Tumbaku Duniani. Kwa kutazama matokeo, haishangazi wanasayansi wanapoilinganisha nikotini na cocaine. Nikotini (nicotine) ni mojawapo ya dawa za kulevya za kale zaidi, inayotumiwa mahali pengi zaidi. Nini maoni ya kisayansi? Anachambua William Shao
Kulingana na Jack Henningfield, mwanasayansi wa Kituo cha Taasisi ya Kitaifa cha Uchunguzi wa Mazoea ya Matumizi Mabaya ya Dawa, Baltimore, Maryland, "...Nikotini hutimiza lengo lile lile linalotimizwa na cocaine ...inasisimua akili za watu kwa njia ile ile ambayo cocaine hufanya."
Kitabu cha Mortality From Smoking in Developed Countries 1950-2000 kilichapisha zaidi ya utafiti 50,000 uliofanywa katika kipindi cha miaka 40 (1953-1993) zinazoonesha kwamba asilimia 87 ya watu wote wanaokufa kutokana na kansa ya mapafu ni wale wanaovuta sigara. Wavutaji wa sigara wana uwezekano wa asilimia 70 ya hatari ya kushambuliwa na magonjwa ya moyo na wanawake wanaovuta sigara 30 au zaidi kwa siku wana uwezekano wa asilimia 74 ya kufa kutokana na kansa ya matiti.
Kinachotisha zaidi katika utafiti huo wa kisayansi, ni ukweli kwamba watoto wanaozaliwa na akina mama wavutaji wa sigara, wanakuwa na tatizo kubwa zaidi la kuwa viziwi. Baya zaidi ni kwamba wagonjwa wa kisukari ambao huvuta sigara wako katika hatari kubwa zaidi ya kuharibika figo zao na kwamba moshi wa sigara hufanya pumu iongezeke zaidi.
Wanasayansi wengine waliochunguza athari za tumbaku na kisha wakaandika kitabu The Scientific Case Against Smoking, walisema uchunguzi mbalimbali wa kansa uliofanywa unaonesha kwamba katika nchi ya Japani, nusu au zaidi ya visa vya kansa ya mapafu vinasababishwa na uvutaji wa sigara.
"Tarakimu za kisayansi zinaendelea kuthibitisha kwamba, upo uhusiano wa karibu kati ya kuvuta sigara na magonjwa ya mapafu na mishipa ya damu," linaripoti gazeti The Herald likimkariri mpasuaji wa kifua katika Idara ya Upasuaji ya Chuo Kikuu cha Zimbabwe, Dk. Douglas Thomson.
Kiasi cha uchunguzi zaidi ya 50 uliofanywa na kuchapishwa, ulihusu watoto zaidi ya nusu milioni waliozaliwa, uligundua kwamba wanawake wajawazito kuvuta sigara kunaathiri sana uzito wa mtoto atakayezaliwa.
"Kuna hatari ya mimba kutoka yenyewe inayofikia asilimia 30 hadi 70 kwa mama wajawazito wanaovuta sigara kuliko wale wasiovuta. Hatari huongezeka kila wakati kulingana na idadi ya sigara zinazovutwa," kinadai kitabu The Health Concequences of Smoking: The Changing Cigarette-A Report of the Surgeon General.
Kitabu hicho kinaongeza: "Watoto wanaozaliwa na wanawake wanaovuta sigara wakati na baada ya uja uzito, hupatwa na kiwango cha juu zaidi cha vifo vya mapema kabla ya umri wa miaka mitano."
Jarida World Health linaripoti, "Ambukizo la kansa kwa watu wengi linaweza kutabiriwa katika nchi nyingi zinazoendelea Tanzania ikiwa miongoni mwake ndani ya miaka kumi ijayo."
Mwaka 1986, ulipofanyika mkutano wa 14 wa kimataifa kuhusu kansa nchini Hungary, wataalamu walikadiria kwamba watu 3,500,000 wangekufa kwa kansa mwaka huo.
Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), milioni moja ya vifo hivyo vingesababishwa na uvutaji sigara. Hata hivyo, makadirio hayo yalizidi ukweli uliojitokeza.
Sir Richard Doll, Profesa mstaafu wa tiba kwenye Chuo Kikuu cha Oxford, alionya kwamba miongoni mwa zile kemikali 3,800 zilizo katika moshi wa tumbako, 50 zimegundulika kuwa zinasababisha kansa kwa wanyama.
Uchunguzi wa nchini Uingereza uliohusu watu wasiovuta tumbako ambao wanaishi na wavutaji, uligundua kwamba kila mtu wa pili aliyekufa kutokana na kansa ya mapafu alikuwa mvutaji moshi wa sigara zilizovutwa na watu wengine.
Timu moja ya utafiti wa tiba katika Chuo Kikuu cha Sydney, Australia, inadai kugundua kwamba kuvuta sigara kunawaumiza sana watoto katika tumbo la uzazi kwa kuwanyima virutubisho vinavyohitajiwa.
Watafiti wamekuwa wakichunguza matokeo ya kuvuta tumbaku kwenye mtiririko wa damu katika kila kiungo kinachounganishwa na mtoto kabla hajazaliwa, chakula anachokula chenye oksijen na kinachoondoa takataka mwilini.
Waligundua kuwa dakika mbili tu baada ya mama kuvuta sigara, ule mtiririko wa damu unapunguza mwendo wake wa kawaida, na matokeo hayo yanaendelea kwa muda wa saa moja hata baada ya mama huyo falaliza kuvuta sigara ya mwisho.
Dkt. Brian Trudinger, Mhadhiri Mkuu katika eneo la utunzaji magonjwa ya akina mama wajawazito, alikiambia kitabu The Health Consequences of Smoking: The Changing Cigarette-A Report of the Surgeon General hivi:
"Kwa wastani, watoto wachanga wa akina mama ambao huvuta sigara kumi kila siku muda wote wa uja uzito wao, wana uzani unaopungua gramu 300 kuliko uzani ule wa watoto wachanga wa wanaozaliwa na akina mama wasiovutaji sigara wakati wa kuzaliwa.
"Kwa njia fulani hii ilisababishwa na mvutaji badala ya uvutaji wenyewe; aina ya mwanamke anayevuta sigara wakati wa uja uzito, huenda alikuwa na matatizo mengine yaliyosababisha kuzaa watoto wadogo zaidi, wenye uzani mdogo zaidi.
"Hata hivyo, utafiti unathibitisha, kuvuta kunaathiri kile mtoto katika tumbo la uzazi la mama yake kwa njia ya moja kwa moja na kupunguza ule mtiririko wa damu kuelekea kwa mtoto hicho..."
Jarida la mambo ya tiba la Uingereza, The Lancet, lilichapisha uchunguzi wa kansa ya utotoni. Uligundua kwamba, kadiri mama anavyozidi kuvuta sigara nyingi kila siku katika kipindi cha ujauzito ndivyo hatari ya kansa kwa mtoto wake atakayemzaa itakavyokuwa kubwa zaidi."
The Lancet linaongeza: "Wakati sehemu zote zenye uvimbe zinapofikiriwa, ile jumla ya hatari ya kansa kwa watoto waliohatarishwa kwa uvutaji sigara kumi au zaidi kila siku katika kipindi cha uja uzito iliongezeka kwa asilimia 50."
Baada ya kuzaliwa, watoto wa wavutaji sigara hupatwa na matatizo hatari zaidi ya afya. Katika toleo lingine la gazeti hilo hilo, iliripotiwa: "Uchunguzi umegundua uhusiano wa moja kwa moja baina ya kuvuta moshi wa sigara na ugonjwa wa pumu tangu utotoni, kuokoteza pumzi kunakoendelea, na magonjwa yanayohusiana na kupumua katika ile miaka ya kwanza na ya pili ya maisha."
Uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Marekani na muhtasari wake ukachapishwa katika gazeti The New York Times, "Wanajeshi wavutaji wa sigara wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupatwa na majeraha wakati wa mazoezi."
Gazeti hilo kudokeza: "Nikotini (sumu iliyoko katika tumbako) hupunguza uwezo wa akili ya mvutaji wakati anapofanya kazi yenye utata ya kutumia akili.
"Madaktari wa akili huamini kwamba sigara zina uhusiano mkubwa na huzuni inayompata mvutaji pamoja na kunyong'onyea kwa ubongo." Kadiri mtu anavyohuzunika ndivyo anavyoelekea kuvuta idadi kubwa zaidi ya sigara.
Jarida The Economist linaitaja sigara kuwa bidhaa inayouzwa kwa wingi zaidi na iliyo na faida kubwa zaidi ikilinganishwa na bidhaa nyingine. Sigara zikitumiwa kama zilivyokusudiwa, huua wateja wake kwa wingi zaidi.
Utafiti wa gazeti hilo, "...Miaka milioni tano ya uhai wa wavutaji wa sigara hupotea kila mwaka nchini Marekani peke yake."
Jarida la Newsweek limechapisha uchunguzi unaofanana na huo, lilipoandika hivi: "Uvutaji wa sigara huua zaidi ya Wamarekani 420,000 kwa mwaka-ikiwa ni karibu mara 50 zaidi kuliko wale wanaokufa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya."
Matokeo ya uchunguzi uliofanywa katika nchi 45 na kuchapishwa katika jarida Reader's Digest la Mei, 1988 unadokeza kwamba, "Duniani pote, watu milioni tatu-ambao ni sawasawa na watu sita kwa kila dakika, hufariki dunia kutokana na uvutaji wa sigara.
"Katika nchi nyingi, hali itaendelea kuwa mbaya zaidi ...Ikiwa mwelekeo wa sasa wa uvutaji sigara utaendelea, basi kutakuwa na vifo milioni kumi kwa mwaka, sawasawa na kifo kimoja kwa kila sekunde tatu."
Kitabu Mortality From Smoking in Developed Countries 1950-2000 kilimkariri Dk. Alan Lopez wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) akisema: "Kuvuta sigara ni moja ya maafa yasiyoweza kulinganishwa na kitu kingine ...hatimaye mmoja kati ya kila wavutaji wawili atakufa kutokana na uvutaji huo."
Uchunguzi wa kitabu hicho uliofanywa katika kipindi cha miaka 40 ulifikia hatua ya kuona, nusu moja ya wavutaji wote wa sigara watauawa na uvutaji.
Uvutaji wa sigara umeongezeka kwa sababu kampuni za sigara hushangilia uhuru wa wanawake. Kampuni za kutengeneza sigara, katika matangazo yao ya biashara, yanadai yanataka kuwasaidia wanawake washerehekee wingi na uhuru walioupata.
Matangazo ya biashara hiyo yanaonyesha picha za wasichana wanaopaswa kuigwa, wakiwa wamepiga picha zao katika mitindo ya kuwavutia wale wengine wasiovuta.
Hata hivyo, Mortality From Smoking in Developed Countries 1950-2000 kinadokeza kwamba: "Idadi ya walioathiriwa na kansa miongoni mwa wanawake imekuwa maradufu katika kipindi cha miaka 20 iliyopita nchini Uingereza, Japan, Norway, Poland na Sweden. Katika nchi za Marekani na Kanada, viwango vimeongezeka kwa asilimia 300 ...lakini tangazo moja la biashara lilidiriki kusema kuwa 'ni maendeleo makubwa'."
Kampuni nyingine za sigara zina mbinu nyingi za kuvutia. Kadiri ya kitabu hicho, kampuni moja ya Ufilipino, katika nchi ambayo idadi kubwa ya watu wake ni Wakatoliki, yalijaribu kuifanya hata picha ya 'Bikira Maria' ihusiane na sigara ili kuwafanya wanawake Wafilipino wasiwe na wasiwasi kuhusu uvutaji wao."
Gazeti China Today linasema asilimia 61 ya wanaume wa makamo huvuta sigara, wakati asilimia saba tu ya wanawake hufanya hivyo. Lakini sasa wanashawishiwa na kampuni ya nchi za Magharibi na ndipo idadi yao inaongezeka.
Kampuni nyingi za nchi za Magharibi huingiza bidhaa zao hizo polepole nchini China, hata hivyo wanakuwa na fursa ndogo mno ya kutangaza bidhaa hiyo.
Kampuni nyingine hutafuta njia ya kujipendekeza kwa wateja wao kiujanja. Kwa mfano, "China ilikuwa ikileta filamu kutoka Hong Kong ambazo waigizaji wake ni wavuta sigara," likasema China Today.
Dkt. Keith Ball anayeshughulikia maradhi ya moyo, Uingereza amekaririwa na gazeti African Health akisema: "Bara la Afrika limeharibiwa na ukame, vita vya wenyewe kwa wenyewe, na ugonjwa wa UKIMW. Ukiachilia mbali vita vya nyuklia au njaa, uvutaji wa sigara ndio tishio kubwa kuliko jambo lingine lolote kuhusu afya za Waafrika."