Post by Yona Maro on Dec 15, 2005 5:51:31 GMT -5
Nakumbuka enzi hizo
Umekaa zako ndani huna hili wala lile muda wa jioni hivi , umepumzika , au unashangaa tu mambo mengine katika TV au Radio .
Ghafla , Baba anakuja , Baba anapenda kuniona nasoma au nafanya kitu kingine na sio kuangalia TV au kusikiliza Muziki , Nilisikia gari ya baba inakuja , huyo mbio kuchukuwa kitabu na kujifanya nasoma , akiondoka au akipita eneo hilo basi kitabu nakiweka pembeni shuguli inaendelea vile vile .
Au akitaka Home work , najua sijafanya basi kazi rahisi naweza kwenda nachora ramani hata ya Tanzania tu naweka mapambo kadhaa ndio nasema hiyo ndio home work yetu .
Siku zingine huna hili wala lile , anakuambia uand**e siku nzima umefanya nini , Kama ulikuwa nyumbani , basi unaweza kusema Nilikuwa na mama shambani tunalima katika maelezo yako , kama ulienda sehemu nyingine lazima itakuwa garage nayo unasema ulichofanya .
Hii ilikuwa kama kiama kwangu , enzi hizo , ukafika wakati sasa baba anatuambia kuhusu maisha , kuhusu sisi kama wanajamii kama binadamu kubadilika na kufuata misingi ya ubinadamu kusoma zaidi , kufanya kazi zaidi , na kufanikiwa zaidi , yote haya wakati fulani tulipuuza , tukaendelea na mipango mengine .
Nikatoka nyumbani kujitegemea , nikawa bado nina hisia za baba alivyokuwa anatuambia , je leo nimefanya nini , ratiba zangu za wiki hii zikoje , nimejifunza nini kipya jinsi ya kufanya kazi kwa mafanikio na kadhalika yote hayo nikafikiria na kuyafuata kwa njia kadhaa .
Katika maisha watu wanakutana na bahati kadhaa , bahati hizi wengi wanazipoteza hasa vijana ambao wanafikiri fulani anayenisaidia au anayenishauri yupo wakati wote ila kuna wakati inabidi uende duniani , huko duniani unakutana na watu wapya sasa unatakiwa utumie mbinu zako na ujanja wako kutokana na mafunzo uliyo yapata
Mie mwaka huu 2005 unaisha nimeona niand**e kuhusu vitu kadhaa mzazi alituambia na kutuonya kuhusu dunia na vituko visa vyake , mara nyingi mtu mzima ndio hujua maisha yanaendaje kwa sababu yeye amepitia enzi hizo , kwahiyo tunawakuwa makini zaidi .
Wakati huu nafikiri mwaka huu nimefanya nini na mambo mengine kadhaa kuhusu mwaka ujao nimefanya vitu kadhaa mfano mradi wa browser ya kiswahili chini ya COSTECH , nimetengeneza na kumiliki website kadhaa kama www.techtz.tk na www.maisha.tk vimeandika kitabu kimoja kuhusu mawasiliano na technologia katika Tanzania , nimeandika makala kadhaa zenye mafanikio katika secta yangu ya Mawasiliano , mtandao na Computer .
Pamoja na mambo mengine , nawashukuru wote walio kuwa nami kwa njia moja au nyingine katika kutekeleza mambo kadhaa katika maisha yangu na kazi zangu kwa mwaka huu wa 2005 zaidi credit ziende kwa ndugu , jamaa , majirani , marafiki , walimu wangu , wafanyakazi wenzangu na wengine wote nilio na ushirikiano nao kwa njia moja au nyingine .
Sote tumekuja duniani na tutaondoka , ni vyema kila mmoja aondoke kwa mafanikio zaidi aliyoyafanya hapa duniani , ambayo alileta faida kwa taifa lake , jamii yake husika yaliyoleta furaha mioyoni mwa watu wake .
Ila nguvu na jitihada ziende zaidi kwa vijana , inaonekana vijana ndio waadhirika na wahanga wakubwa wa mambo yote machafu na mabaya katika dunia hii , mfano Magonjwa kama UKIMWI na kadhalika .
Nakutakia Weekend Njema