Post by Yona Maro on Dec 11, 2005 6:40:59 GMT -5
VYAMA vyetu vya siasa takribani 18 vimejitosa katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu unaofanyika Desemba 14, mwaka huu.
Huu ni Uchaguzi Mkuu wa tatu chini ya mfumo wa siasa wa vyama vingi ulioanza nchini mwaka 1992. Uchaguzi wa kwanza katika mfumo huu, ulifanyika mwaka 1995 ukafuatiwa na ule wa mwaka 2000.
Awali uchaguzi huu ulipangwa kufanyika Oktoba 30, mwaka huu, lakini ukasimamishwa hadi Desemba 18. Mabadiliko haya yalitokana na kifo cha aliyekuwa Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Jumbe Rajabu Jumbe kilichotokea Oktoba 26, siku chache kabla ya siku ya uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), iliamua kubadilisha siku ya uchaguzi ili kukipa nafasi CHADEMA kumtafuta Mgombea Mwenza wa kuziba nafasi iliyoachwa na Marehemu Jumbe na pia, kutoa muda wa pingamizi na uandaaji na usambazaji wa karatasi za kupigia kura majimboni.
Katika hali isiyohitaji ubishi, kubadilishwa kwa tarehe hiyo hadi Desemba 18 ambayo pia imebadilishwa na kuwa Desemba 14, mwaka huu, kulilalamikiwa na wanasiasa wengi kwa kuwa kwa vyovyote, kumeathiri mwitikio wa wapiga kura.
Aidha, mabadiliko haya ingawa yamefanyika kwa mujibu wa Katiba na mazingira halisi, yamevibebesha vyama vya siasa mzigo mzito kiuchumi kwani, tangu awali vilikwishajiwekea bajeti inayozingatia uchaguzi kufanyika Oktoba 30 na izingatiwe kuwa, havina fungu maalumu kwa ajili ya kampeni kutoka serikalini.
Kwa upande wa Tanzania Visiwani (Zanzibar), uchaguzi ulifanyika kama ulivyopangwa na matokeo yameiweka CCM madarakani kwa kumchagua Amani Abed Karume kuwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi. Kazi sasa imebaki katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wabunge na madiwani.
Kwa mang'amuzi yangu, hiki ni kipindi kigumu kwa vyama na huu sasa ni uchaguzi mzito na usiotabirika kwa kuwa kutokana na mwenendo wa kampeni, hakuna chama kinachoweza kusema kwa dhati kwamba kitashinda.
Hii ni kutokana na vyama vingi kujitosa katika ngoma hii ya uchaguzi ili navyo vijue matamu na machungu ya mfumo wa demokrasia ya namna hii huku kila kimoja kikilenga ukombozi wa Mtanzania. Hili ni jambo jema.
Si siri huu ni uchaguzi mzito na mkubwa kwa sababu ni uchaguzi unaoiondoa madarakani Awamu ya Tatu na kuiweka Awamu ya Nne na pia, kama Watanzania walivyozoea kunyonya busara na hekima za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, uchaguzi huu tangu mwanzo wa mchakato wake, unafanyika bila kuwapo kwa Mwalimu aliyekuwa mwongozo safi wa Watanzania.
Kama ilivyo kwamba kila mwana na mbeleko yake na kila pepo huja kwa mvumo wake, ndivyo ilivyo pia kwamba, kila chama vikiwamo vile kumi vilivyosimamisha wagombea wa urais; kila kimoja kinatumia mbinu zake kushawishi Watanzania wakipe ridhaa.
Vipo vinavyotumia helikopta, sawa kabisa huo ni ubunifu. Vipo pia vinavyotumia nyimbo na wasanii mbalimbali kuvutia watu kwenye mikutano huku kukiwa na matukio ya kushawishi kupigiwa kura; hakuna ugomvi; ruksa.
Pia, vipo vyama ambavyo vinaendeleza falsafa ya kwamba, simba mwenda kimya, ndiye mla nyama na zaidi, miongoni mwa vyama hivyo, vipo pia vinavyosema ukweli na vinavyoongopa kuhusu wafuasi wa vyama vingine kurudisha kadi na kujiunga navyo; hayo yapo. Mradi tu, katika uchaguzi, kuna mengi.
Ninasema hivyo kwani mwitikio wa Watanzania kuhusu mageuzi ya kisiasa, unaonekana sasa; kwamba Watanzania wanataka mageuzi, lakini wanakatishwa tamaa na mwelekeo unaooneshwa na baadhi ya vyama hususan vya upinzani.
Wengi walitarajia katika uchaguzi wa mwaka huu, vyama vya upinzani vitazingatia usemi kuwa 'umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu'. Badala yake, wanachokishuhudia sasa kinaonesha kuwa karibu vyama vyote vinaamini na kujigamba eti vinakubalika.
Kwa mang'amuzi yangu, mwenzio akinyolewa, wewe tia maji. Nasema hivyo nikiamini kuwa, uchaguzi uliofanyika Zanzibar, umeonesha kuwa, kwa kila mtu kuamini kuwa ndiye anayekubalika kukalia kiti cha Ikulu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kubaki mikononi mwa CCM.
Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. Nani alijua kuwa CUF ikisimama peke yake Visiwani itaambulia kujitangazia matokeo na kuandamana barabarani, lakini isilikanyage zulia la Ikulu?
Kwa manga'muzi yangu, Mungu ana njia nyingi za kuwatumia watu wake, ingawa halazimishi kuzitumia. Nasema hivyo nikiamini kuwa, yaliyotokea hata uchaguzi kuahirishwa, hayakutokea kwa bahati mbaya. Najua kibinadamu, kuondokewa na mwenzetu ni bahati mbaya, hilo halina ubishi, lakini kwa Mungu, ni mpango maalumu wenye lengo maalumu maana kazi ya Mungu haina makosa.
Kwangu mimi, kuahirishwa kwa uchaguzi huenda ni karata nyingine Mungu ameitoa kwa Watanzania hususan wana mageuzi, kujitafiti makosa yao na kuyarekebisha japo Waingereza wanasema 'no easy task' (hakuna kazi rahisi).
Wapinzani waione nafasi hii kama golden chance; wakae haraka wajadiliane namna ya kushika Dola kwa ustaraabu bila kujali ni chama gani; watafute kwanza Dola kutoka Chama Tawala; hiyo ndiyo iwe hatua ya kwanza.
Hatua ya pili, baada ya kufanikisha hilo, sasa waangalie katiba inasemaje kuhusu mgawanyo wa madaraka na ikibidi kurekebisha Katiba kwa maslahi ya umma, irekebishwe au kubadilishwa kabisa.
Yote haya yafanyike yakiongozwa na dhamiri safi kwa kila mmoja. Ugonjwa wa kila mmoja kusema anakubalika eti kwa kuwa anatumia njia hii au ile kukusanya watu wengi katika mikutano, au kudanganyika na ushabiki, nauona kama nuksi na sumu inayokwaza mageuzi ya kweli nchini.
Kwa mang'amuzi yangu, bila wapinzani kupata hekima, busara na ujasiri wa kuungana na kuachiana majimbo kwa dhati na kwa ushirikiano kuungana mkono, wataendelea kubaki kama mapandikizi ya Chama Tawala kuua upinzani, lakini ndoto ya kuikanyaga Ikulu isitimie katu.
Hivi nani asiyejua namna vyama vya upinzani vilivyopata nguvu kwa sasa, tazama CUF, tazama CHADEMA, tazama NCCR-Mageuzi, tazama TLP na vingine. Kisha, tazama namna Chama Tawala kilichoongoza nchi kwa miaka 44 sasa; kilivyo na nguvu. Hivi wapinzani wameshindwa kuliona hilo na kuungana ili kukitoa madarakani Chama Tawala?
Inashangaza kwani hii inaonesha vyama vingi havilengi mageuzi yenye lengo la ukombozi wa Mtanzania, bali ajenda na manufaa binafsi. Nani asiyejua umuhimu wa kuungana ili kufikia lengo? Tazama Kenya walipoamua, mbona iliwezekana kukitoa chama tawala madarakani?
Kabla sijaenda mbali, ninavipongeza sana baadhi ya vyama vilivyoungana na kumsimamisha mgombea mmoja; sina sababu ya msingi kuvitaja. Hivyo vimefanya jema.
Nionavyo mimi, viongozi wetu wa vyama vya siasa vya upinzani, wengi wametawaliwa na ubinafsi na uchu wa madaraka, ndiyo maana wanahadaiwa na watu wanaokuja kwenye mikutano yao.
Hao, wanafikiri kuwa ni wote wanaokuja kwenye mikutano hiyo, ndio watakaowachagua na wala hawajui kuwa, hata ndani ya vyama vyao, wapo ambao hawatachagua wagombea kutoka vyama vyao.
Kwangu mimi, mwamko unaoonekana katika kampeni hizi, ndicho kilikuwa kipindi muhimu cha wapinzani kuingia Ikulu, lakini bahati mbaya, penye miti hakuna wajenzi. Hilo hawalioni na wanachoona, ni ubinafsi wa kila mtu kutaka aitwe Rais. Ndiyo maana kumbe vyama vingi, wenyeviti ndio wagombea wa urais kana kwamba chama ni Mwenyekiti pekee; hakuna wengine.
Sishindwi kusema kwa ujasiri kwamba, ndiyo maana hata viongozi wengine wameamua kuona kwamba, bila wao kugombea, chama hakipo na pengine, hawajui labda wao ndio tatizo, hivyo wawaachie wengine wajaribu vipaji vyao.
Wazungu wanao usemi kuwa, 'charity begins at home', yaani wema huanzia nyumbani. Kwa kukataa kuungana, wapinzani wanalionesha hilo? Kwa mtaji huo wanashindwa nini kutamka kuwa wana sera za ubinafsi? Kama katika kugombea wameonesha hayo, vipi wakichukua madaraka? Si kwamba nchi itaongozwa kwa jazba na majigambo ambayo hayatasaidia kitu?
Udhaifu ambao wapinzani wanauonesha japo bado wana nafasi ya kuurekebisha hauoneshi kuwa wana lengo la kumkomboa Mtanzania kiuchumi, kijami na kidemokrasia, bali kujikomboa wenyewe.
Hivi kwa kuungana na kuachiana majimbo kwa dhati, nani atatarajia Bunge lijalo kuwa na wabunge wanaoburuzwa na chama kimoja hata kama itafikia hatua ya kudanganyana kwa kupiga kura dhidi ya hoja fulani?
Tunapenda Bunge lijalo, liwe na changamoto ya nguvu za hoja si hoja za nguvu. Bunge mchanganyiko lina faida nyingi. Hakuna kulala. Hakuna kuogopana bali kunakuwa na kuheshimu nguvu ya hoja.
Kwa kushindwa kuungana, wapinzani wajue wanatumia mikono na kura za watu wao wenyewe kukifanya Chama Tawala kiendelee kushika hatamu ama kwa kujua, au kwa kutojua. Na ndiyo maana baadhi yao wanadaiwa kuwa ni mapandikizi wa CCM.
Wanasiasa wajue kuwa unafiki wanaoufanya wa kujiona maarufu na wanaokubalika wakasaini hata mikataba bila kutafakari vyema, kisha baadaye wakaongoza malalamiko na kugomea matokeo, ni hali inayoonesha ukengeufu wa hali ya juu.
Wapinzani mnachemsha bila nyinyi wenyewe kujua, lakini bado nafasi ya masahihisho na kujirekebisha ipo. Mungu anawapenda ndiyo maana amewapa nafasi nyingine ya kujirekebisha. Kubalianeni kuungana na kuachiana majimbo, kisha mwone matunda mtakayochuma uchaguzi ukifika. Simamisheni mgombea mmoja kitaifa na katika kila jimbo; mtacheka na kushangilia huku mkinywa asali na maziwa Krismasi na Mwaka Mpya.
Mtaingia madarakani na Bunge litakuwa na wabunge mchanganyiko watakaoweza kujadili hoja bila woga, bali kwa manufaa ya umma mzima wa Watanzania. Mtajikuta kila chama kina wajumbe wa kutosha bungeni na hii, itawapa nguvu ya ruzuku ili mwendeleze vyama vyenu na kuvijenga zaidi.
Kinyume cha hayo, matokeo ya uchaguzi uliofanyika Zanzibar, ni rasharasha, masika yenyewe myasubiri Desemba 14; mtaona mtakavyosherehekea Krismasi kwa huzuni huku CCM wakiimba zile nyimbo zao. Hapo, Watanzania hatutapenda kuona wala kusikia malalamiko na kuchochea kuni za vurugu wala maandamano maana penye miti hakuna wajenzi.
Hivi kweli mmekubali kuwa heri wapinzani mshindwe wote mrudi mitaani kwa kuwa kifo cha wengi ni harusi? Zingatieni kuwa, majuto ni mjukuu na kwamba, ajidhaniaye amesimama, aangalie asinguke. Ijulikane kuwa, ingawa kifo cha wengi ni harusi, lakini kaburini anaingia mmoja mmoja na ndivyo kila mgombea anavyorudi peke yake kwa chama chake.
Vyama vya upinzani vizingatie kuwa, havijachelewa sana; bado vina nafasi ya kufanya marekebisho na kisha, nyadhifa katika idara na wizara nyeti, vikagawana. Badilikeni kutoka katika ubinafsi mwingie katika umoja; mtafurahia sikukuu ya Krismasi ya mwaka huu. Mtaonesha ukomavu wenu na Watanzania wataona matunda ya mageuzi ya kisiasa.
Kumbukeni Watanzania wengi hawakuwa na imani na mfumo wa vyama vingi, lakini kumbukeni namna mlivyowashawishi na sasa wanawaelewa na kuwafuata, lakini kwa nini jema la kuunganisha nguvu mnalikataa na kuhusudu ubinafsi?
Kwa mang'amuzi yangu, kama nafasi, sheria na taratibu zilizobaki zinaruhusu, tumieni muda uliobaki kurekebisha kosa la kutoungana. Vinginevyo, mtashindwa kurudisha majibu kwa wanachama, wapiga kura na wafadhili wenu na badala yake, mtaamua kuchochea vurugu ili ionekane kwamba uchaguzi umevurugika kumbe ni aibu ya namna ya kurudi kwa wananchi na wafadhili kutokana na kosa la uzembe wa ubinafsi na kujidhani kila mmoja amesimama.
Kwa Mungu sina kosa, jukumu langu la kusema nimetimiza, atakayesikia na asikie na asiyetaka na aache, lakini maneno yangu mtayakumbuka.